missiochorheaderver6

(Tafadhali bonyeza "WEITERLESEN")  

Chor3BHistoria fupi kuhusu Kwaya yetu

Umoja wa Madaktari wa Wamisionari wa Hospitali ya Wamisionari Wurzburg hapa Ujerumani, walikusanyika pamoja na kuanzisha kikundi kiitwacho KWAYA YA WAMISIONARI. Kwaya hii inaimba na kucheza muziki wa Nyimbo za injili kutoka barani Afrika. Kikundi hiki kipo chini ya Uongozi na usimamizi wa Mwimbaji mahiri Dr. Bi. Renate Geiser (Daktari wa matibabu ya Ndani na Mwalimu wa Muziki).
Kwaya hii ya Wamisionari (Missio Choir), ilianzishwa mnamo mwaka 1994. Kwaya hii ilianzishwa kutokana na upendo wetu wa Nyimbo za dini Kutoka Afrika, kwani ni wenye nguvu na uhai hata unapousikiliza.

Nyimbo Zetu

Nyimbo nyingi zimekusanywa na Mwalimu wa Mziki Dr. Bi. Renate Geiser, akishirikiana na waimbaji wengineo waliokuwa wakifanya safari zao kwenda Afrika na ambao walipata nafasi ya kuhudhuria Ibaada za Jumapili au maonyesho ya kitamaduni. Dr. Bi. Renate alishirikiana nao kuziandaa upya nyimbo hizo na kuzifundisha kwa wanakwaya wengine.

Waimbaji toka Afrika

Waimbaji toka Afrika wanatusaidia sana kutufundisha nyimbo mpya toka nchi mwao. Pia tunapata nafasi ya kuweza kujifunza lugha zao, tamaduni mbali mbali, mitindo ya miziki na jinsi wanavyocheza.

Kikundi cha wapiga Ngoma-Ensemble - TROMMELHAUS-Ensemble

Muziki wetu unasindikizwa na ngoma toka Kikundi cha wapiga Ngoma-Ensemble (TROMMELHAUS-Ensemble). Kikundi hiki kinacheza ngoma za Kiafrika. Pia ni wabunifu mahiri wa midundo mbali mbali ya ngoma.
Kwaya yetu inaumahiri wa kuimba na kucheza Muziki wa nyimbo za Dini kutoka nchini Kenya, Tanzania, Congo, Ethiopia, Sudan, Senegal, Ghana, Togo, Guinea, Afrika Kusini, Nigeria na Zimbabwe. Kwa njia tunmeweza kupata kujua utamaduni barani Afrika.

KWAYA YA WAMISIONARI (MISSIO CHOR) na KIKUNDI CHA WAPIGA NGOMA (TROMMELHAUS-Ensemble), huimba pamoja katika ibaada mbali mbali mjini Würzburg na katika vitongoji vyake. Kutokana na uimbaji wetu, kurekodi na kuuza CD zenye nyimbo nzuri, twaweza kusaidia miradi ya mahosiptali na ya kijamii barani Afrika. KWAYA YA WAMISIONARI (MISSIO CHOR) pia inasaidia miradi ya Catholic Institute for International Health.

Kwa maelezo zaidi tuandikie:
Anwani ya Barua pepe
Diese E-Mail-Adresse ist vor Spambots geschützt! Zur Anzeige muss JavaScript eingeschaltet sein!

Dr. Renate Geiser
Missionsärztliches Institut Würzburg
Salvatorstraße 7
97074 Würzburg
Ujerumani

(photos: Ignas Kawedi Shayo)

­